Ajira

Mambo ya Kutarajia

1. Ombi lako
Kutoka kwenye orodha iliyo kwenye ukurasa wetu wa Search Jobs, tafuta nafasi inayolingana na utaalamu wako na malengo yako ya kazi. Ili kuanza mchakato wa kutuma ombi, nenda kwenye maelezo ya kazi na, chini ya ukurasa, tumia kitufe cha Apply for This Position kuwasilisha wasifu na barua ya maombi. Utapokea barua pepe ya uthibitisho tutakapozipokea.

Iwapo sifa zako zitakidhi mahitaji yetu, tunaweza kuwasiliana nawe ili kupanga mahojiano ya simu na mmoja wa wafanyakazi wetu wa upataji vipaji. (Angalia folda yako ya barua taka usipoona jibu.) Kwa sababu ya idadi kubwa ya maombi, hatuwezi kuwajibu waombaji wote.

2. Mahojiano yako ya simu
Mmoja wa wafanyakazi wetu wa upataji vipaji atakupigia simu kujadili historia yako ya ajira na sifa zako. Pia atafafanua mchakato wa Rotary wa kuajiri na kujibu maswali yoyote uliyo nayo kuhusu kufanya kazi Rotary.

Baada ya simu, tutakujulisha ikiwa umechaguliwa kuendelea katika mchakato wa kuajiri. Ikiwa ndivyo, tutapanga hatua inayofuata. Kwa baadhi ya nafasi, utaombwa kufanya jaribio la ujuzi au kukamilisha kazi.

3. Mahojiano yako ya ana kwa ana
Wakati wa mahojiano yako, tutauliza kuhusu maarifa yako, ujuzi wako na mambo unayopenda. Timu zetu za kuajiri hutumia mbinu za mahojiano ya kitabia ili kutusaidia kuchagua mgombea anayefaa kwa kazi. Tunataka kuhakikisha kuwa nafasi hiyo inakufaa na kwamba wewe unaifaa nafasi hiyo.

Pia utapata nafasi ya kuuliza maswali kuhusu kazi na kuhusu Rotary. Tunakuhimiza kutembelea Rotary.org mapema ili ujifamishe na kazi yetu.

Mazingira ya ofisi ya Rotary ni ya mavazi ya kikazi yasiyo rasmi sana.

4. Nini kinachofuata
Iwapo umechaguliwa kwa nafasi hiyo, mmoja wa wafanyakazi wa Upataji Vipaji ataomba marejeleo ya kitaaluma na kufanya ukaguzi wa usuli.

Ikiwa hujachaguliwa, utajulishwa baada ya nafasi kujazwa. Rotary na mahitaji ya jamii tunazohudumia hubadilika kila wakati, kwa hivyo tunakuhimiza kupitia ukurasa wetu wa Search Jobs mara kwa mara kwa nafasi nyingine zinazolingana na ujuzi na uzoefu wako.

5. Uelekezaji wako
Rotary inajivunia kuunda mazingira ya ukaribisho kwa wafanyakazi wote. Siku yako ya kwanza, utakuwa na mpango wa uelekezaji wa mfanyakazi mpya unaoeleza mafunzo yako ya kuanza kazi. Mafunzo haya yameundwa kukusaidia kujifunza kuhusu utamaduni na sera za Rotary. Msimamizi wako na timu yako mpya watatoa mafunzo na msaada wa ziada.
 


Je, uko tayari kuchunguza kazi na Rotary?
 

Nenda kwenye ukurasa wa kutafuta kazi ili upate nafasi inayolingana na uzoefu na maslahi yako.

Loading component...