Vilabu vya Rotary vya Kenya vinapanda mbegu na kutafakari matunda ya kazi yao

Wanachama wa Rotary wanaboresha maisha kupitia miradi endelevu ya kilimo, wakisaidia jamii kulima chakula na kuongeza kipato.

by Rotary International
3 May 2021

Loading component...

Klabu ya Rotary ya Muthaiga inastawi

22 Mei 1997

Ilipata hati rasmi ikiwa na wanachama 38

Leo

wanachama 59

“Kila rais huja na ajenda yake mwenyewe,” Bomett anasema. “Nilipoingia, nilitaka mazingira yawe jambo kuu la kuzingatiwa. Mazingira ni muhimu.” Miaka michache iliyopita, klabu ilifanya kazi na vilabu vingine kadhaa vya Rotary na Rotaract, pamoja na Mamlaka ya Barabara za Mijini ya Kenya na serikali ya eneo hilo, kupanda takriban miti 3,000 jijini; wanachama sasa wanashirikiana na Huduma ya Misitu ya Kenya katika mradi mwingine, mkubwa zaidi. “Wakati huu, tunataka kupanda mara tatu ya tuliyopanda awali,” Bomett anasema.

“Sisi ni klabu imara sana,” Bomett anasema. “Tuna historia nzuri ya miradi na msingi mzuri wa mtaji kwa upande wa fedha zetu. Tuna idadi nzuri ya watu katika uongozi, na tumewaleta watu wanaofaa. Rotary Club of Muthaiga ina msukumo mkubwa.”

Hadithi hii ilichapishwa awali katika toleo la Mei 2021 la Rotary magazine.

Loading component...