Mojawapo ya desturi za Rotary zenye rangi nyingi zaidi ni wanachama kubadilishana mabango ya klabu. Klabu huonyesha mabango yao ya mapambo kwenye mikutano na hafla za wilaya, na mara nyingi Warotari wanaosafiri kwenda nchi nyingine hubeba mabango haya ili kubadilishana na klabu wanazotembelea.
Mara nyingi mabango hayo hujumuisha alama au picha za mji, eneo, au nchi ya klabu. Baadhi huwakilisha desturi za kitamaduni za eneo au ustadi wa kisanaa kwa kuonyesha kazi za ngozi, ususi, urembaji wa taraza, au michoro iliyopakwa kwa mkono. Mengi ya mabango hayo ni kazi za sanaa yenyewe.
Kubadilishana mabango kulipopata umaarufu mkubwa, Bodi ya Wakurugenzi ya Rotary International ilihofia kuwa desturi hiyo ingeweka mzigo wa kifedha kwa klabu. Mwaka 1959, iliwahimiza wanachama “kutumia busara, kiasi, na uamuzi wa makini” wanapoandaa ubadilishanaji huo.
Leo, desturi hii inaendelea kama njia ya klabu kuonyesha urafiki wao.
Takribani mabango 20,000 katika kumbukumbu za Rotary yanaonyesha fahari ya klabu kuhusu miji yao ya asili na uhusiano wao na Rotary International.


